Jarida la michezo la nchini Ufaransa
linalofahamika kama Le Parisien limeandika kuwa winga wa klabu ya Manchster
United Angel Di Maria amekubali kujiunga na klabu ya PSG ya nchini Ufaransa.
Kwa mujibu wa jarida hilo,usajili wa Angel Di
Maria utakuwa wa pauni milioni 45 pamoja na mchezaji mmoja toka PSG ambaye ni
beki wa kulia Gregory Van Der Wiel.
Kwa muda mrefu sasa Di Maria amekuwa
akihusishwa na kujiunga na vilabu vya Bayern Munich, Arsenal na PSG kutokana na
kufanya vibaya msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment