Winga wa klabu ya Liverpool Raheem Sterling
ameshindwa tena kufanya mazoezi na timu yake ya Liverpool hii leo.
Taarifa zaidi zinasema kuwa mchezaji huyo bado
anasema kuwa anaumwa na hakufanya mazoezi.
Hapo jana Sterling alishindwa kufanya mazoezi
na wenzake kwa kusema kuwa anaumwa na taarifa zikazidi kusema kuwa mchezaji
huyo hatojiunga na timu kwa maandalizi ya msimu ujao wa Ligi ambayo yataanzia nchini Thailand.
Daktari toka Liverpool alikwenda kuangalia
Afya yake na kupendekeza aina ya matibabu anayopaswa kufanyiwa Raheem Sterling.
Kwa muda mrefu sasa mchezaji huyo amekuwa
akihusishwa na kujiunga na klabu ya Manchester City.
0 comments:
Post a Comment