Timu zinazoshiriki michuano ya Sports Xtra Ndondo Cup hatua
ya makundi zimekabidhiwa vifaa tayari kwa ajili ya hatua hiyo inayotarajiwa
kuzinduliwa siku ya ijumaa.
vifaa hivyo vimekabidhiwa leo kwa viongozi wa timu hizo
mbele ya mdhamini wa mashindano hayo Dr. Juma Mwaka wa kituo cha Foreplan
Clinic.
Waratibu wa mashindano hayo Clouds Media Group kupitia
kwa mkuu wa kitengo cha michezo Shaffih Dauda, amesema lengo la kuanzisha
mashindano hayo ni kuwapa vijana nafasi ya kuonesha vipaji vyao na kujiepusha
na vitendo vya kihuni.
Kwa upande wake mdhamin wa michuano hiyo Dr Juma Mwaka
amesema uamuzi wake wa kudhamini mashindano hayo ni kutokana na michezo hivi
sasa kuwa ajira.
Mashindano hayo hatua ya makundi yatazinduliwa siku ya
ijumaa katika uwanja wa Bandari Tandika kati ya mabingwa watetezi Abajalo fc ya
Sinza dhidi ya Kauzu Fc ya Tandika sokoni.
Kama ilivyo mwaka jana bingwa atajinyakulia kitita cha
shilingi million tano, mshindi wa pili million 3, na mshindi wa tatu million 2,
huku kikundi bora cha ushangiliaji kikiondoka na milioni moja.
0 comments:
Post a Comment