Timu
ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania wenye umri chini ya miaka 20
(Tanzanite) itashuka dimbani siku ya jumamosi katika uwanja wa Azam
Complex kucheza na timu ya U20 ya Zambia (The Young She-polopolo) katika
mchezo wa kwanza kuwania kufuzu kwa fainali za U-20 za Dunia mwaka
2016.
Mechi kati ya Tanzanite dhidi ya Young She-Polopolo kuwania
kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya miaka 20
itachezwa katika uwanja wa Azam Complex - Chamazi majira ya saa 10
kamili jioni.
Kikosi cha timu ya Tanzanite chini ya kocha wake
mkuu Rogasian Kaijage iliyoweka kambi eneo la Mbande na kufanya mazoezi
yake katika uwanja wa Azam Complex kwa takribani wiki ya pili sasa
kujiandaa na mchezo huo.
Hali ya kambi ya Tanzanite ni nzuri
wachezaji wote wapo katika hali nzuri na morali ya ya hali ya juu,
kikubwa Watanzania wanaombwa kujitokeza kwa wingi siku ya jumamosi kuja
kuwapa sapoti timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 watakapokuwa
wakicheza na wenzao wa Zambia.
Nayo timu ya Taifa ya U20 ya
Zambia Young She-polopolo inatarajiwa kuwasili kesho alhamis jioni kwa
usafiri wa ndege wa shirika la Rwanda Air ambapo ijumaa wanatarajiwa
kufanya mazoezi katika uwanja wa Azam Complex.
Mchezo huo
utachezwa siku ya jumamosi majira ya saa 10 kamili jioni katika uwanja
wa Azam Complex - Chamazi, ni wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Dunia za
Wanawake chini ya miaka 20 (U-20) zitakzofanyika nchini Papua New
Guninea mwaka 2016.
Mwamuzi wa mchezo huo ni Batol Mahjob kutoka
nchini Sudan, akisaidiwa na washika kibendera Remaz Osaman na Walaa
Bilal, mwamuzi wa akiba Khadmallah Elasayed wote kutoka nchini Sudan na
Kamisaa wa mchezo ni Flora Roosevelt kutoka nchini Malawi.
Wakati
huo huo Kikundi cha ushangiliaji cha timu za Taifa (Taifa Supporters)
kimejiandaa kwenda kuwapa sapoti timu ya Tanzanite siku ya jumamosi
katika mchezo dhidi ya The Young She-Polopolo uwanja wa Azam Comlpex.
Taifa
Supporters baadaya kikao cha viongozi wa wao wamepanga kuwa na kikundi
cha ushangiliaji cha watu wasiopungua 150 (mia moja hamsini) katika
mechi hiyo ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Dunia kwa Wanawake chini ya
miaka 20.
Wanchama wa kikundi cha Taifa Supporters watakutana
jumamosi saa 5 kamili asubuhi kisha kuelekea uwanja wa Azam kwa ajili ya
kuwashangilia Tanzanite katika mchezo huo.
Wapenzi wa mpira wa
miguu, wadau mnaombwa kujitokeza siku ya jumamosi kuwapa sapoti
Tanzanite katika mchezo wao wa awali dhidi ya Zambia, kabla ya mchezo wa
marudaino utakaofanyika tarehe 25 Julai, 2015 Lusaka nchini Zambia.
Taarifa na afisa habari TFF
Wednesday, July 8, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment