Friday, January 25, 2013
BABA AMBAKA MWANAE WA MIAKA 6 MKOANI NJOMBE
Licha ya kuwepo adhabu kali kwa watu wanajihusisha na vitendo vya ubakaji, bado vitendo hivyo vimeendelea kushamiri katika maeneo mbalimbali nchini ambapo wilayani Njombe mtu mmoja amefikishwa mahakamani akituhumiwa kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 6.
Kesi hiyo ambayo imevuta hisia za watu wengi, imesomwa mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya ya Njombe, Isack Mlowe na mwendesha mashataka wa polisi Henry Chaula, Januari 24 mwaka huu.
Mwendesha mashata huyo ameiambia mahakama kuwa mshtakiwa aliyefahamika kwa jina la Leonald Mapile mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa kijiji cha Idunda kata ya Kifanya Wilayani humo alitenda kosa hilo januari 22 majira ya saa 7 mchana.
kamanda wa polisi mkoa wa njombe Fulgency Ngonyani
Imedaiwa kuwa Mapile alimwingilia kimwili mwanaye na kumsababishia majeraha makubwa sehemu za siri, ambapo amekana mashtaka hayo na kupelekwa mahabusu katika gereza la Mpechi hadi februari 6 mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment