Friday, January 25, 2013
KICHANGA KINGINE CHATUPWA DAMPO MTAA WA VIBANDA VYA CCM MKOANI IRINGA
picha kutoka maktaba
Siku chache baada mtoto mchanga kutupwa katika bonde la mto maeneo ya chuo kikuu cha Tumaini mkoani Iringa, tukio la aina hiyo limetokea tena mkoani humo baada ya mtoto mwingine anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja kutupwa katika dampo la takataka.
Mtoto huyo anayedaiwa kutupwa leo majira ya saa 3 asubuhi ameonekana na akina mama wanaozoa takataka katika dampo hilo kwenye vibanda vya CCM mtaa wa mashine tatu katika Manispaa ya Iringa.
Akizungumza katika eneo la tukio, mwenyekiti wa mtaa huo, Dotto Majaliwa, mbali ya kulaani kitendo hicho amewashauri wanawake wenye tabia hizo kutumia njia za uzazi wa mpango ili kuepuka na mauaji hayo.
Kwa upande wao baadhi ya mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio licha ya kulaani kitendo hicho, pia wameshangazwa na hatua ya mwanamke aliyemtupa mtoto huyo wakisema kitendo hicho hakifai katika jamii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment