SHIRIKISHO
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo lilisimamisha mchakato wa
uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na
baadhi ya wagombea kulalamika kuenguliwa sasa litatuma ujumbe wake
nchini katikati ya mwezi ujao.
Ujumbe
huo ambao moja ya shughuli zake kuwasikiliza wote walioenguliwa na
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF na hawakuridhika na uamuzi huo,
utakuwepo nchini Aprili 16 na 17 mwaka huu.
Kwa
mujibu wa barua ya Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke kwenda kwa Rais
wa TFF, Leodegar Tenga, kazi ya ujumbe huo ni kubaini tatizo lililopo na
kutoa ripoti kwa mamlaka zinazohusika ndani ya FIFA kwa ajili ya kutoa
mwongozo.
Ujumbe
huo utakutana na pande mbalimbali zinazohusika wakiwemo wagombea,
kamati za uchaguzi za TFF. Lakini pia ujumbe huo unatarajia kumtembelea
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara
pamoja na watendaji wake wizarani.
Uchaguzi
wa viongozi wa TFF ulikuwa ufanyike Februari 24 mwaka huu, lakini
ukasimamishwa na FIFA baada ya baadhi ya wagombea walioenguliwa
kulalamika kuwa hawakutendewa haki na wangependa shirikisho hilo
liingilie kati.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment