Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu na Bunge, Bw. William Lukuvi katikati akizunguza katika mkutano wa Majadiliano ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership Dialogue) uliofanyika Mkoani Iringa na Kushirikisha makundi ya wananchi kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Capt. Aseri Msangi na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Bw. Raymond Mbilinyi na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro, ambapo majadiliano hayo yalikuwa yanalenga kupata maoni ya wananchi juu ya matumizi ya sayansi na teknolojia katika uzalishaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu na Bunge, Bw. William Lukuvi katikati akibadiliashana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (kushoto) na kulia kwake ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa la Biashara TNBC, Bw. Raymondi Mbilinyi na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) katika majadiliano ya Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Smart Partnership Dialogue) uliofanyika mkoani Iringa na kuyashirikisha makundi ya wananchi kutoka mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe.
0 comments:
Post a Comment