Meneja Mauzo na Masoko wa Oxford University Press
Bi.Fatma Shangazi(kulia)akimuonesha Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina
Nkurlu (kushoto) na Meneja maendeleo ya kibiashara wa kampuni hiyo Asia Mhina, moja
ya vitabu vinavyouzwa kwenye banda lao katika
viwanja vya maonesho ya 37 ya biashara
ya kimataifa (sabasaba) wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya kampuni yake
na Vodacom utakao wawezesha wateja kutumia huduma ya M PESA kununua vitabu.
Meneja maendeleo
ya kibiashara wa kampuni ya Oxford University Press, Asia Mhina (kushoto) na Meneja
Mauzo na Masoko wa kamnpunoi hiyo Bi.Fatma Shangazi(kulia)wakifatilia neno kutoka kwa Meneja wa
Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu katika moja ya Kamusi ”Dictionary” zinazouzwa
kwenye banda lao katika viwanja vya maonesho ya 37
ya biashara ya kimataifa (sabasaba)
wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya kampuni yake na Vodacom utakao
wawezesha wateja kutumia huduma ya M PESA kununua vitabu.
Meneja Mauzo na Masoko
wa Oxford University Bi.Fatma Shangazi(kulia)akiwaonesha waandishi wa habari
(hawapo pichani) moja ya vitabu vinavyouzwa kwenye banda lao katika viwanja vya maonesho ya 37
ya biashara ya kimataifa (sabasaba) wakati
wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni yake na Vodacom utakao wawezesha
wateja wanaotumia huduma ya M PESA kununua vitabu, wanaoshuhudia kutoka kushoto
ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina
Nkurlu na Meneja maendeleo ya kibiashara
wa kampuni hiyo Asia Mhina.
Ili kuongeza
kasi ya usomaji wa vitabu kwa watanzania suala ambalo limekuwa ni changamoto
kubwa hapa nchini kampuni ya Oxford University
Press imeingia ubia na Vodacom Tanzania ili kuwawezesha wateja mbalimbali
kununua vitabu kupitia huduma ya M pesa, Vitabu vitakavyo weza kununuliwa na
kuuzwa ni pamoja na vile vya kiada na Ziada kutoka katika kampuni hiyo.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa Ushirikiano huo uliofanyika katika maonesho ya 37 ya Sabasaba
Meneja Ukuzaji Biashara wa Vodacom Asia Mhina amesema kuwa kutokana na kukua zaidi kwa
huduma ya M-Pesa hapa nchini pamoja na
kuepuka usambazaji kwa wateja wa Oxford ndiyo sababu iliyosababisha wao kuingia
ubia huo.
Mhina
alibainisha pia ubia huo umekuja katika wakati muafaka kwa ajili ya kuwarahisishia
wateja wa vitabu kuepukana na foleni zilizopo kwenye mabenki pamoja na kuokoa
muda wa malipo kwa wateja pia kuongeza kasi ya ununuaji na usomaji wa vitabu
kwa Watanzania.
“Lengo la huduma
hii ni kuwarahisishia wateja na wananchi kufanya malipo ya vitabu kwa urahisi ,
pia kuongeza kasi ya ununuaji na usomaji wa vitabu kwa Watanzania suala ambalo
limekuwa ni changamoto kubwa sasa, hivyo hatua hii itawezesha kukabiliana na
changamoto hizo,” alisema Mhina na kuongeza kuwa,
“Mteja wa
Vodacom sasa atalipia vitabu hivyo kwa njia rahisi zaidi ambapo akitaka kufanya
malipo atafungua orodha ya M pesa kama kawaida na kisha kuchagua malipo na
kuweka namba ya biashara ya Oxford ambayo ni 870870 na kisha kufanya malipo.”
Kwa upande
wake meneja masoko wa Oxford Fatma
Shangazi alisema kuwa huduma ya malipo ya
vitabu kwa M-Pesa itawarahisishia wateja wao kufanya malipo kwa urahisi pasipo
usumbufu wowote wala kupoteza muda na pia itawaweka katika hali ya usalama
zaidi.
“Tunafurahi
kuingia katika ubia na kampuni ya Vodacom ni hatua kubwa kwetu na tunaamini
kuwa ushirikiano huu utakuwa chachu ya kuongeza hali ya usomaji wa vitabu kwa
Watanzania, alisema Shangazi.
0 comments:
Post a Comment