Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed
Shein amesema kuwa ni dhima ya Waislamu kutilia mkazo suala la kuishi
pamoja kama ndugu katika misingi ya kuheshimiana, kustahamiliana na
kupendana, kama Uislamu unavyofundisha.
Amesema kuna kila sababu kwa
Waislamu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema anazowapa kila uchao.
Sambamba na hayo, Dk Shein amewakumbusha Waislamu kuswali na kuwa na
njia bora za kutumia mali walizojaliwa na Mungu na kuzidi kukumbushana
na kuhimizana kutoa zaka na sadaka.
Rais wa Zanzibar amewataka Waislamu
kutayarisha nafsi zao kuupokea Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ambao husogeza
pepo karibu zaidi na waja wa Mwenyezi Mungu.
Dkt Shein amewahimiza
Waislamu kujiepusha na Israfu wakati wa Ramadhani na pia kuwataka
wanabiashara kutoongeza kiholela bei ya bidhaa muhimu wakati wa mfungo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment