Viongozi wa nchi tatu za Amerika ya Latini wamesema wako tayari kumpa
hifadhi mfanyakazi wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Marekani NSA
Edward Snowden ambaye amefichua taarifa kuhusu mradi mkubwa wa ujasusi
wa Marekani kote duniani.
Bolivia imejiunga na Venezuela na Nicaragua
ambazo zimesema ziko tayari kuma hifadhi Snowden.
Rais Evo Morales wa
Bolivia amesema atampa hifadhi Snowden kama njia ya kulalamikia hatua ya
nchi za Ulaya ya kuizuia ndege yake iliyokuta ikitoka Moscow kwa madai
kuwa ilikuwa imembeba Snowden.
Morales amesema nchi za Ulaya ziliizuia
ndege yake kwa amri ya Marekani.
Snowden, hivi karibuni alifichua kwamba
Marekani imekuwa ikidukua mitandao ya intaneti na kukusanya taarifa za
siri za watu kote duniani; jambo ambalo ni kinyume na sheria za
kimataifa.
Snowden pia alifichua kwamba mashirika ya kijasusi ya
Marekani ya CIA na NSA yamekuwa yakinasa mazungumzo ya simu kote
duniani.
Aidha alifichua kuwa Marekani imekuwa ikiwafanyia ujasusi
maafisa wa kidiplomasia wa nchi za Umoja wa Ulaya jambo ambalo limeibua
hasira kote Ulaya.
Snowden hivi sasa amepata hifadhi ya muda katika
uwanja wa ndege Moscow jambo ambalo limepelekea kuzorota uhusiano wa
Marekani na Russia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment