KITABU cha kwanza nchini kinachozungumzia soka la Tanzania
kijulikanacho kwa jina la “Soka la Tanzania” kitaanza kuuzwa siku ya mechi ya
watani wa Jadi, Yanga na Simba iliyopangwa kufanyika Jumamosi kwenye uwanja wa
Taifa.
Akizungumza na jijini jana, mtunzi wa kitabu hicho, Katibu
Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Kandanda nchini (TFF), Fredrick Mwakalebela
alisema kuwa maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika na yamedhaminiwa na kampuni TSN Group kupitia kinywaji chake
cha kuongeza nguvu Chilly Willy, Events World, Vannedrick Tanzania Limited na Inbox Pub.
Wadhamini wengine ni Clouds FM, Times FM na Street Soul kwa
mujibu wa Mwakalebela. Alisema kuwa kwa sasa ametoa nakala 10,000 kwa ajili ya
kuuzwa Tanzania nzima.
Alisema kuwa kitabu hicho kimezungumzia historia ya soka
la Tanzania katika Nyanja za vijana, wanawake na wanaume, ligi kuu ya Tanzania
Bara, Taifa Cup, Timu ya Taifa na Utawala Bora.
Mbali ya hayo, kitabu hicho kimezungumzia ujio wa kocha
Marcio Maximo, mchango wa serikali katika kuinua mpira wa miguu, wadhamini,
uhusiano kati ya waandishi wa habari na TFF na changamoto mbali mbali za mpira
wa miguu Tanzania.
“Pia nimeelezea mambo niliyojifunza chini ya Rais Leodegar
Tenga kwa kipindi cha miaka mine nikiwa TFF, matatizo niliyokutana nayo kutoka
kwa makamandoo na kuniita mimi muimba kwaya wakati wa utambulisho wangu wa
kwanza Juni 15, 2006,” alisema
Mwakalebela.
Alisema kuwa kitabu hichi ni muhimu sana kwa wana-habari,
wachezaji, makocha, waamuzi na wadau wengine wa mchezo huo kwani kuna
kumbukumbu zote za mechi za timu ya Taifa ikiwa mabao ya kufunga, wafungaji,
vikosi tofauti vya timu za taifa na mambo mengine.
TAARIFA HII KWA HISANI YA ROCKETSPORTS
0 comments:
Post a Comment