Main Menu

Wednesday, May 15, 2013

SOMA HADITHI HII UNAWEZA KUJIFUNZA KITU NA KUBADILIKA

Chumba Cha Siri
Ni siku nyingi kidogo, mwaka 1979, lakini ni
tukio ambalo liliniuma sana. 


Ilikuwa vigumu
sana kulisahau na lilinifanya nijiulize, inakuwaje
Mungu anakuwa mkatili kiasi kile. Lakini bila
shaka ilikuwa ni wakati ule wa ufahamu mdogo.



Hivi sasa ninafahamu mengi na hasa baada ya
kujifunza maarifa haya ya utambuzi.
Ilikuwa ni mwaka 1979 nikiwa nasafiri kutokea
Dar es salaam kwenda Arusha. 


Sijui ilikuwaje,
lakini ilitokea. Tuliondoka Dar es salaam saa
12.30 jioni. Wakati ule mabasi yalikuwa yakisafiri
jioni na usiku, sio kama siku hizi.


Nilikuwa ninakwenda Arusha kwenye usaili kwa
ajili ya ajira, nikiwa ndio kwanza nimemaliza
kidato cha nne. 


Niliajiriwa moja kwa moja
serikalini, kwani siku zile ajira zilikuwa ni za
kumwaga. 


Hata hivyo sikuridhishwa na kazi
niliyokuwa nafanya, hivyo niliomba kazi kwenye
kampuni moja kule Arusha na niliitwa kwa usaili.


Tulifika mji unaoitwa Korogwe ambao wakati ule
ulikuwa ndio mji maarufu kwa hoteli zake katika
barabara yote ya Segera hadi Moshi na Arusha.



Tulipofika Korogwe basi letu lilisimama kwa ajili
ya abiria kupata chakula. Niliingia kwenye hoteli
moja ambayo nakumbuka hadi leo kwamba
ilikuwa ikiitwa Bamboo. 


Niliagiza chakula na kula
haraka kutokana na muda mfupi wa kula
uliotolewa na wenye basi la TTBS ambalo ndilo
nililosafiri nalo.


Wakati wa kulipa ndipo niliposhangaa na
kuogopa. 


Niliingiza mkono mifukoni na kukuta
kwamba sikuwa na hela. 


Nilianza kubabaika na
mwenye hoteli alisema hawezi kukubali ujinga
huo, "Abiria wengine wahuni bwana, anakula na
kujifanya kaibiwa, ukikubaliana nao kila siku
hasara tu" Mwenye hoteli alisema kwa
kudhamiria hasa.



Kulizuka zogo kubwa, huku mwenye hoteli
akisema ni lazima anipeleke polisi. 


Ni kweli
alimtuma mmoja wa watumishi wake kwenda
kituo cha polisi ili nishughulikiwe…
­…

 
 Hapo Hotelini kulikuwa na bwana mmoja
aliyekuwa amekaa pembeni na mkewe na
watoto wao wakila. 
 
Yule bwana alipoona vile
alimtuma mhudumu mmoja aniite. Niliondoka
pale kaunta nilipokuwa nabembeleza na kuja
kwa yule bwana.

Alikuwa ni kijana mtu mzima kidogo, mwenye
miaka kama 50 hivi. Nilimsalimia na aliitikia,
nilimsalimia mkewe pia. Yule bwana aliniuliza
kisa cha vurugu ile na nilimsimulia. 
 
Aliniuliza
sasa huko Arusha ningeishi vipi wakati wa usaili
wakati nimeibiwa fedha zote na ningerudi vipi
Dar. Nilimwambia nilikuwa napanga namna ya
kurudi Dar, kama huko polisi ningeaminika.

Kama mzaha vile yule bwana aliniambia kuwa
angenipa fedha za kutumia huko Arusha na
nikirudi Dar nimrudishie fedha zake.

Nakumbuka alinipa shilingi 90 kwa ahadi
kwamba nikirudi Dar nimpelekee fedha zake
ofisini kwake. 
 
Alinielekeza ofisini kwake, mtaa wa
Nkuruma na kuniambia kuwa ameamua
kunisaidia kwa sababu kila binadamu anahitaji
msaada wa mwingine na maisha haya ni
mzunguko. 
 
Nilimshukuru na kuondoka
kukimbilia basini. Basi lilikuwa linanisubiri mimi
tu. Nilipanda ndani ya basi na abiria wengine
walinipa pole. 
 
Tuliondoka Korogwe, lakini
haikuchukua muda basi letu lilipata tatizo la
pancha ya gurudumu moja la mbele. Ilibidi
tuegeshe pembeni ili litengenezwe. 
 
Baada ya
matengenezo, tuliondoka kuendelea na safari
yetu.

Karibu na mji wa Same kwenye saa saba usiku,
basi letu lilisimama ghafla. 
 
Abiria walisimama
ndani ya basi na kulizuka aina ya kusukumana.
Huko nje kulikuwa na ajali. Abiria tulishuka
haraka na wengine huko chini walishaanza
kupiga mayowe, hasa wanawake. 
 
Niliposhuka
niliona gari ndogo nyeusi ikiwa imebondeka
sana na hapo kando kulikuwa na maiti wawili.

Nilijua ni maiti kwa sababu walikuwa
wamefunikwa gubigubi. Halafu kulikuwa na
katoto kalikokuwa kanalia sana kakiwa
kamefungwa kanga kichwani. 
 
Tumwahishe
huyu mtoto hapo Same hospitali ameumia,
ingawa sio sana. Nilikatazama kale katoto ka
kiume kenye umri wa miaka kama mitatu.

Kalikuwa kameumie kwenye paji la uso, lakini
kalikuwa hai. Bila shaka wale walikuwa ni wazazi
wake, kalikuwa yatima tayari. Machozi
yalinitoka.

Baada ya kupata msaada na askari wa usalama
barabarani kuchukua maiti wale tulipanda basini
kuendelea na safari yetu. 
 
Kale katoto
kalichukuliwa na jamaa fulani waliokuwa na
Land Rover ya serikali kukimbizwa hospitalini.
Ndani ya Basi mazungumzo yalikuwa ni kuhusu
ajali ile tu, hadi tunafika Arusha. 
 
Tulichelewa
sana kufika Arusha kwani tulifika kwenye saa
tano asubuhi, badala ya saa mbili .

Nililala kwenye hoteli rahisi na kufanya usaili
kesho yake. Ni hiyo kesho, baada ya usaili
niliponunua gazeti ambapo nilipata mshtuko
mkubwa ajabu. 
 
Kumbe wale watu wawili
waliokufa kwenye ajali ile ya Same walikuwa ni
yule bwana aliyenisaidia hela na mkewe. 
 
Yule
mtoto wao ndiye aliyeokoka. Niligundua hilo
baada ya kusoma jina lake na jina la kampuni
aliponiambia nimpelekee fedha zake nikirudi
Dar, pamoja na picha yake, mke na mtoto. Nililia
sana, kama mtoto.

Nillishindwa kujua ni kwa nini afe. Nilijiuliza ni
nani sasa angemlea mtoto yule? Yalikuwa ni
maswali yasiyo na majibu na pengine maswali
ya kijinga pia.

Nilijua kwamba nilikuwa na deni, deni la shilingi
tisini. Kwa wakati ule shilingi tisini zilikuwa ni
sawa na shilingi laki moja za sasa.
Kwa mara ya kwanza sasa nilijiuliza ni kwa nini
marehemu yule aliniamini nakuamua kunipa
fedha zile. Sikupata jibu.
Nilikata kipande kile cha gazeti la kingereza
kilichokuwa na habari ile. 
 
Nilichukuwa kipande
hicho na kukiweka kwenye Diary yangu. Deni,
Ningelipa vipi deni la watu? Nilijikuta nikipiga
magoti na kuomba mungu anipe uwezo wa kuja
kulilipa deni la mtu yule mwema kwa njia
yoyote. 'Mungu naomba uje uniwezeshe kulilipa
deni la marehemu kwa sura na namna ujuavyo
wewe. Nataka kulilipa deni hili ili nami niwe
nimemfanyia jambo marehemu,' niliomba.
Nilirejea Dar siku hiyo hiyo.
 
Kwa sababu ya
mambo mengi na hasa baada ya matokeo ya
usaili ule kuwa mbaya kwangu, nilijikuta nikiwa
na mambo mengi na kusahau haraka sana
kuhusu mtu yule aliyenisaidia mbaye ni
marehemu. 
 
Nilifanikiwa hata hivyo kupata nafasi
ya kusoma Chuo cha Saruji na baadae chuo cha
ufundi na hatimaye nilibahatika kwenda nchini
Uingereza. Mwaka 1991 nilianza shughuli
zangu.
Ilikuwa ni mwaka 1995 nikiwa ofisini kwangu
pale lilipokuwa jengo Nasaco ambalo liliungua
mwaka 1996, ambapo lilijengwa upya na
kubadilishwa jina na kuitwa Water Front. 
 
Nikiwa
nafanya kazi zangu niliambiwa na sekratari
wangu kwamba kulikuwa na kijana aliyekuwa
anataka kuniona. Nilimuuliza ni kijana gani,
akasema hamjui. 
 
Nilimwambia amruhusu aingie.
Kijana huyo aliingia ofisini. Alikuwa ni kijana
mdogo wa umri miaka kama 17 au 18 hivi,
mweupe mrefu kidogo. 
 
Alikuwa amevaa bora
liende , yaani hovyohovyo huku afya yake ikiwa
hairidhishi sana.

Nilimkaribisha ilimradi basi tu, kwani niliona
atanipotezea bure muda wangu. Ni lazima niwe
mkweli kwamba sikuwa mtu mwenye huruma
sana na nilikuwa naamini sana katika watu
wenye pesa au majina. Nilimuuliza, “nikusaidie
nini kijana na ukifanya haraka nitashukuru
maana nina kikao baada ya muda mfupi”.
Nilisema na sikuwa na kikao chochote , lakini
nilitaka tu aondoke haraka.

“Samahani mzee, nilikuwa na shida…..nimefuk
uzwa shule na sina tena mtu wakunisaidia kwa
sababu …..nime….niko ….kidato cha pili na hivyo
tu natafuta tu kama atatokea mtu……..
Nilimkatisha. “Sikiliza kijana. Kama huna jambo
lingine la kusema, ni bora ukaniacha nifanye
kazi. Hivi unafikiri kama nikiamua kumsaidia kila
mtu aliyefukuzwa shule si nitarudi kwetu kwa
miguu! Nenda Wizara ya Elimu waambie……
Kwanza wazazi wako wanafanya kitu gani, kwa
nini washindwe …..Kwa nini walikupeleka shule
ya kulipia kama hawana uwezo, wanataka sifa?”
“Hapana wazazi wangu walikufa na ninasoma
shule ya serikali. 
 
Nimekosa mahitaji ya msingi na
nauli ya kwendea shule. Nasoma shule ya Kwiro,
Morogoro. Shangazi ndiye anayenisomesha,
naye ana kansa na hivi sasa hata kazi
hafanyi….,” Alianza kulia. 
 
Huruma fulani ilinijia
na nilijiambia, kama ni nauli tu na matumizi,
kwa nini nisiwe mwema, angalau kwa mara
moja tu. “Baba na mama walifariki lini?” Niliuliza
nikijua kwamba, watakuwa wamekufa kwa
ukimwi, maana kipindi kile ndipo fasheni ya
ukimwi ilipoanza, ambapo kila anayekufa
huhesabiwa kwamba kafa kwa ukimwi.
“Walikufa kwa ajali nilipokuwa mdogo sana,
nilipokuwa na miaka mitatu. Ndio shangazi
yangu akanichukua na kunilea hadi sasa
anakufa kwa kansa.” Yule kijana alilia zaidi.

Naomba nikwambie wewe msomaji unayesoma
hapa kwamba, kuna nguvu fulani na sasa
naamini kwamba ziko nyingi ambazo huwa
zinaongoza maisha yetu bila sisi kujua.
Kitu fulani kilinipiga akilini paaa! Nilijikuta
namuuliza yuel kijana. 
 
“Kwa nini umeamua kuja
kwangu, ni nani alikuelekeza hapa na wazazi
wako walikufa mwaka gani na wapi?”
Yule kijana alisema, “Nimeona nijaribu tu kwa
mtu yeyote ambaye anaweza kunisaidia, na ndio
nimejikuta nikiingia hapa, sijui……..sikutu
­mwa
na mtu. 
 
Wazazi wangu walikufa mwaka 1979
huko Same na mimi wanasema nilikuwa kwenye
ajali, nikaokoka. Niliumia tu hapa.” Alishika
kwenye kovu juu ya paji lake la uso.

Nilihisi kitu fulani kikipanda tumboni na kuja
kifuani halafi niliona kama vile nimebanwa na
kushindwa kupumua. 
 
“Baba yako alikuwa
anaitwa nani?” “Alikuwa anaitwa
Siame….Cosmas Siame….” Niliinuka ghafla hadi
yule kijana alishtuka . 
 
Nilikwenda kwenye kabati
langu mle ofisini na kuchakura kwenye droo
moja na kutoka na diary. 
 
Mikono ikinitetemeka,
nilitoa kipande cha gazeti ndani ya diary hiyo,
nilichokuwa nimekihifadhi.

“Ndio alikuwa anaitwa Cosmas Siame. Huyu ni
mtoto wake, ni yule mtoto aliyenusurika.”

Nilinong’ona. Nilijikuta nikipiga magoti na kusali.
“Mungu, wewe ni mweza na hakuna
kinachokushinda
­. 
 
Nimeamini baba kwamba kila
jema tunalofanya ni akiba yetu ya kesho na
kesho hiyo huanzia hapa duniani.” Halafu
nillinyamaza na kulia sana. 
 
Nililia kwa furaha na
ugunduzi wa nguvu zinazomgusa binadamu
kwa kila analofanya.

Nilisimama nikiwa nimesawajika kabisa. Nilihisi
kuwa mtu mwingine kabisa. Nilimfuata yule
kijana na kumkumbatia huku nikiwa bado
ninalia. “Mimi ni baba yako mdogo, ndiye
nitakyekulea sasa. 
 
Ni zamu yangu sasa kukulea
hadi mwisho” Naye alilia bila kujua sababu na
alikuwa amechanganyikiw
­a kabisa. 
 
Nilirudi
kwenye kiti na kumsimulia kilichotokea miaka
17 iliyopita.

Tuliondoka hapo na kwenda kumwona shangazi
yake Ubungo, eneo la maziwa ambako alikuwa
amepanga chumba. 
 
Kutokana na hali yake
nilimhamishia kwangu, baada ya kumsimulia
kilichotokea. 
 
Huyo dada yake Cosmas alifurahi
sana hadi akashindwa kuzungumza kwa saa
nzima. Alifariki hata hivyo mwaka mmoja
baadae, lakini akiwa ameridhika sana.

Kijana Siame alisoma na kumaliza Chuo Kikuu na
hivi sasa yuko nchini Australia anakofanya kazi.

Ukweli ni kwamba ni mwanangu kabisa sasa.

Naamini huko waliko Mbinguni wazazi wake
wanafurahia kile walichokipanda miaka
mingisana nyuma. 
 
Lakini nami najiuliza bado.
Ilikuwaje Cosmas akanipa msaada ule? Halafu
najiuliza ni kitu gani kilimvuta mwanae Siame
hadi ofisini kwangu akizipita ofisi nyingine zote?
Nataka nikuambie, usiwe mbishi sana bila
sababu, kuna nguvu za ziada zinazoongoza
matokeo maishani mwetu…………
*************MW
­ISHO***********­ *********
Namalizia kwa kusema haya
Life can be tough. But at least we have food.
Right? Hot food and lots of it. At least we have a
home. Right? A warm bed, pillows and blankets.
At least we have clothes. Right? Lots of clothes
in fact. At least we have parents, siblings,
people who love, protect us. Right? No matter
how tough OUR lives are, there's always
someone out there in a worse situation. Let's
pray for them too. Please press share to spread
this important message

0 comments:

Post a Comment