Main Menu

Wednesday, May 15, 2013

MWIZI WA VITHIBITI MAHAKAMANI MKOANI IRINGA AKAMATWA SAMBAMBA NA SISTER FEKI




                           Sister feki Phylis Wanjiru Kamau


JESHI la polisi mkoa wa Iringa limemkamata mwanamke Phylis Wanjiru mwenye umri wa miaka 44 aliyevalia mavazi ya kitawa wa masister wa kanisa Kathoriki, ambapo baada ya kupekuliwa amekutwa na baadhi ya vielelezo vilivyobaini kuwa ni tapeli.

Wanjiru ambaye ni raia wa nchi ya Kenya amekamatwa na jeshi la polisi baada ya masister wenzie kubaini kuwa si mmoja wao, kutokana na kushindwa kufanya baadhi ya masuala  ambayo ni msingi wa utawa wao.

Akizungumzia mkasa huo, kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda amesema mwanamke huyo kabila laKe ni Muwembu wa nchini Kenya amekamatwa katika nyumba  za masista zilizopo Ipogolo mjini Iringa.

Aidha Kamuhanda amesema mwanamke huyo ambaye awali aligoma kutoa maelezo ya kina juu ya ujio wake nchini Tanzania, katika upekuzi walimkuta na baadhi ya chip (Line) za makampuni mbalimbali ya simu ya ndani na nje ya nchi.

Kamuhanda amesema Sister huyo bandia alikutwa pia akiwa na hati za kusafiria (Passport) mbili, moja ikiwa niya Africa Mashariki yenye namba Ke. 020659 huku hati ya nyingine ikiwa na jumuiya ya Kenya namba A. 1790366.

Amesema Sister huyo feki katika hati hizo ilionyesha kuwa alitembelea nchi ya Rwanda, Uganda pamoja na nchini Tanzania ambapo siku za hivi karibuni alikuwa Mkoani Mara Tarime.

Sister huyo FEKI amekuwa akitumia mbinu ya kujiangusha kama mtu mwenye ugonjwa wa kifafa pindi anapofanyiwa mahojiano, jambo linalowawia vigumu jeshi hilo kupata maelezo ya kina dhidi ya dhamira yake ya kuingia humu nchini.

Kamuhanda ameitaka jamii kuwa makini na wageni mbalimbali, huku akiwaasa kuacha tabia ya kuwaamini watu kwa muonekano wao, kutokana na mwanamke huyo kutumia njia hiyo ambayo inamfanya kila mtu kumuamini.

&&&&&&&&&&&&&&&&&

Katika tukio lingine jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikiria mtumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa kwa tuhuma za kuiba vielelezo vya madawa ya kulevya aina ya bangi.

Kamuhanda amesema tukio hilo limefanyika tarehe 14  ambapo mtuhumiwa huyo wa mahakama  Lwitiko Lusekelo Minga ambaye ni mlinzi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa, aliiba bangi yenye uzito wa kg 371.2

“Tukio la kupatikana kwa bangi, eneo la Flerimo mtuhumiwa Juma Nzowa alikamatwa na bangi na baada ya kuhojiwa mtuhumiwa alimtaja Lwitiko Lusekelo Minga Mlinzi wa Mahakama kuwa ndiye aliyemuuzia kielelezo hicho cha mahakama,” Alisema Kamuhanda.

Pia amesema kielelezo hicho awali kilikamatwa Wilaya ya Kilolo na kufikishwa mahakamani kama ushahidi na ndipo ilipoibiwa tena.

Amesema kutokana na uwepo wa watumishi wasio waaminifu kumekuwa na tabia hiyo hasa kwa madawa hayo ya kulevya, vielelezo vyake na kurudi tena mitaani huku wao wakiendelea na zoezi la kukamata.

Hata hivyo kumekuwa na malalamiko mbalimbali juu ya vielelezo hivyo kuibiwa pindi vifikapo Mahakamani, hasa kwa vidhibiti hivyo vya madawa ya kulevya na  vipodozi mbalimbali ambapo huuzwa katika maduka na wananchi kuendelea kutumia.

Aidha vielelezo kama vyombo vya thamani navyo vimesemekana mara nyingi hupotelea Mahakamani na hata katika vituo vya Polisi.

kwa msaada wa olivermotto.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment