Timu
ya Taifa ya Morocco (Lions of the Atlas) inatarajiwa kuwasili nchini
keshokutwa Ijumaa kwa ndege ya Emirates tayari kwa mechi ya mchujo ya
Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Jumapili
katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Msafara
wa timu hiyo yenye watu 58 wakiwemo maofisa 19 na waandishi wa habari
12 utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa
8.55 mchana na utafikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency.
Siku
hiyo Morocco inatarajia kufanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, na Jumamosi itafanya mazoezi yake ya mwisho kwenye
Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa saa 9 kamili
alasiri.
Wachezaji
walioko kwenye kikosi hicho chini ya Kocha Rachid Taoussi ni Nadir
Lamyaghri, Anas Zniti, Yassine Bounou, Younnes Bellakhadar, Abdellatif
Noussair, Abderrahim Achchakir, Zoheir Feddal, Younnes Hammal, Zakarya
Bergdich na Abdeljalil Jbira.
Issam
El Adou, Kamel Chafni, Salaheddine Saidi, Mohamed Ali Bamaamar,
Abdelaziz Barrada, Salaheddine Aqqal, Abdessamad El Moubarky, Nordin
Amrabat, Chahir Belghazouani, Abdelilah Hafidi, Youssef Kaddioui, Brahim
El Bahri, Hamza Abourazzouk na Youssef El Arabi.
Wakati
huo huo, tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa kesho
katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo,
mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha
Mafuta Buguruni, Uwanja wa Taifa na Dar Live Mbagala.
Milango siku ya mechi kwa ajili ya watazamaji itafunguliwa saa 6 kamili mchana.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
0 comments:
Post a Comment