Tuesday, March 26, 2013
BOEING YAANZA MAJARIBIO YA NDEGE ZAKE 787
Kampuni kubwa ya kutengeneza ndege aina ya Boeing Aerospace, imefanya jaribio la kwanza la kurusha ndege zake za Boeing 787 Dreamliner, baada ya tatizo la betri kutatuliwa.
Jaribio la saa mbili lililofanywa jana Jumatatu, limefanyika vizuri kama lilivyokuwa limepangwa na kampuni hiyo.
Ndege za Boeing 787 Dreamliner, zilisitisha safari zake mwezi Januari, mwaka huu, baada ya ndege zake mbili kugundulika zilikuwa na hitilafu katika betri zake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment