Rais wa zamani wa Afrika kusini Nelson Mandela
anasemekana kuwa hali yake inaendelea vizuri baada
ya kuwapo hospitali kwa muda wa siku tisa sasa.
Rais
Jacob Zuma amesema kuwa Mandela ameendelea
kuwa pamoja na familia yake katika hospitali ya mjini
Pretoria ambako anapatiwa matibabu.
Katika hotuba,
Zuma pia alitoa wito wa watu kujiunga nae ili
kumtakia Mandela siku njema ya maadhimisho ya siku
ya kinababa.
Mandela mwenye umri wa miaka 94
anasumbuliwa na maambukizi katika mapafu, ikiwa ni
mara ya nne kulazwa hospitalini kwa ajili ya matibabu
tangu Desemba mwaka jana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment