KOCHA wa Manchester United, David Moyes
amepeleka ujumbe kwa Chelsea kwamba Wayne Rooney hatahamia Stamford
Bridge majira haya ya joto kufuatia mchezo wa jana wa miamba hao
uliomalizika kwa sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Rooney alianza katika kikosi cha kwanza
baada ya tetesi za muda mrefu majira haya ya joto kwamba atajiunga na
Jose Mourinho Magharibi mwa London, lakini alipiga soka ya uhakika
akiwa na uzi mwekundu.
Rooney akimdhibiti Ramires |
Katika mchezo huo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Enlgand baina ya timu hizo, United ilianzisha washambuliaji watatu, Welebeck, Rooney na Van Persie.
Dakika ya 65 Lampard alishika kabisa mpira kwenye eneo la hatari kufuatia shuti la Cleverley, lakini refa 'akapeta'.
Dakika ya 71 Ashely Cole alianguka
kwenye eneo la hatari wakati akikabiliana na Jones na akalilia penalti
na hata Mournho akaonekana kulalamika akiwa kwenye benchi.
Mchezo ulikuwa mkali na timu hizo zilishambuliana kwa zamu na baada ya mechi wachezaji walipongezana kwa mchezo mzuri.
Jose Mourinho alisema baada ya mechi
mchezo ulikuwa wa haki na hadhani kama kuna iliyomzidi mwenzake uwezo,
wakati Moyes alilalamikia penalti ya Lampard kuunawa mpira na
kuwapongeza vijana wake kwa soka nzuri.
Kikosi cha Man United kilikuwa: De Gea,
Jones, Ferdinand, Vidic, Evra, Valencia/Young dk67, Cleverley, Carrick,
Welbeck/Giggs dk78, Rooney na Van Persie.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Ramires, Lampard, De Bruyne/Torres dk60, Oscar, Hazard/Azpilicueta dk93 na Schurrle.
Amerudi kikosi cha kwanza: Rooney
alianza katika kikosi cha kwanza na alicheza vizuri akipiga mashuti
mazuri mawili yaliyokaribia kuzaa mabao Old Trafford
Rafu: Cole akimchezea rafu RVP
Cole akimdhibiti RVP
Mpira wa mikono? Lampard akiwa ameshika
mpira kwa mikono ndani ya eneo la hatari na refa hakutoa penalti, ingawa
anashuhudia tukio hapo
Kipa? Lampard alibeba majukumu ya kipa wake dakika ya 65
Alijirusha? Cole alianguka kwenye eneo la hatari na kulilia penalti, wakati akikabiliana na Jones
Analilia penalti: Kocha Jose Mourinho akilalamika baada ya Cole kuanguka na refa hakutoa penalti
Zama mpya, kocha mpya: Moyes akiiongoza United leo baada ya kurithi mikoba ya Sir Alex Ferguson mwishoni mwa msimu
Mapokezi mazuri; Moyes akisaini karatasi za mashabiki
Rooney anatakiwa na Chelsea, lakini leo alipandishwa kikosi cha kwanza
Cole akikabiliana na Rooney
Mourihno na Moyes wakisalimiana kabla ya mechi Old Trafford
0 comments:
Post a Comment