Timu
za African Sports ya Tanga na Mwadui FC ya Shinyanga zinatrajiwa kucheza mchezo
wa fainali ya kusaka Bingwa wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) siku ya jumapili
katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
African
Sports waliibuka washindi wa kwanza katika Kundi A, na Mwadui FC washindi wa
kwanza Kundi B watacheza mchezo huo wa fainali ambapo Bingwa atapewa zawadi ya
Kombe na medali, hali kadhalika kwa msindi wa pili.
Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) ilimalizika mwishoni mwa wiki kwa timu nne kupanda Ligi
Kuu kwa kila kundi kutoa timu mbili, Kundi A ni African Sports na Majimaji FC,
Kundi B ni timu za Mwadui FC na Toto Africans.
Nazo
timu za Green Worriors na Villa Squad zimeteremka Daraja la pili baada ya
kushika nafasi za mwisho kwenye msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza, Villa Squad
kutoka Kundi A na Green Warriors Kundi B.
TAIFA
STARS KUCHEZA NA KOMBAINI YA TANGA LEO
Timu
ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa miguu (Taifa Stars Maboresho) leo inatarajiwa
kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya kombani ya jiji la Tanga katika
Uwanja wa Mkwakwani.
Mchezo
huo wa kujipima nguvu ni sehemu ya program ya kocha mkuu Mart Nooj ya kupata
nafasi ya kuona maendeleo ya wachezaji wake ambao anawaandaa kuwa wachezaji wa
timu ya Taifa ya baadae.
Mara
baada ya mechi ya leo jioni jijini Tanga, timu hiyo itarejea jijini Dar es
salaam ili kutoa fursa kwa wachezaji kujiunga na vilabu vyao kwa ajili ya
michezo inayowakabili mwishoni mwa wiki ikiwemo Ligi Kuu ya Vodacom na Fainali
ya Ligi Daraja la Kwanza.
0 comments:
Post a Comment