Timu ya Mwadui kutoka mjini Shinyanga jana imetawazwa kuwa
Mabingwa wapya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kuifunga timu ya African
Sports ya jijini Tanga kwa bao 1 - 0, katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Azam
Comlex Chamazi jijni Dar es alaam.
Bao pekee na la ushindi kwa timu ya Mwadui lilifungwa na
mshambulaji Kelvin Sabato Kongwe dakika ya 53 ya mchezo na kuihakikishia Mwadui
ushindi katika mchezo huo wa fainali.
Mabingwa hao wapya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
walizawadia Kombe la Ubingwa, medali pamoja na hundi ya sh.millioni tatu, huku
timu ya African Sports ikipata medali na hundi ya sh. millioni 2.
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF linaipongeza timu ya
Mwadui kwa kuibuka Bingwa mpya wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa
2014/205.
Jumla ya timu nne zimepanda Ligi Kuu msimu ujao ambazo
ni Bingwa Mwadui FC, African Sports,
Majimaji na Toto Africans.
0 comments:
Post a Comment