Rais wa Shrikisho
la Mpira wa Miguu nchini –TFF Bw Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa Mwenyekiti
wa Kamati ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer), Bw. Ahmed Mgoyi kwa ushindi wa
jumla wa mabao 12- 9 dhidi ya timu ya Taifa kutoka nchini Kenya.
Timu ya Taifa ya
Tanzania ya Sola la Ufukweni, mwishoni mwa wiki iliibuka na ushindi wa mabao
7-6 katika mchezo uliofanyika kwenye Ufukwe wa klabu ya Escape 1 eneo la
Msasani Jijini Dar es salaam.
Katika salamu zake
Bw. Malinzi amesema ushindi walioupata timu ya soka la Ufukweni mwishoni mwa
wiki, umeitangaza vizuri nchi ya Tanzania na kuwataka Viongozi wa soka la
Ufukweni, makocha, wachezaji kutobweteka na ushndi huo, zaidi kujipanga kwa
maandalizi ya mchezo utakaofuata.
Baada ya kuitoa
timu ya Taifa ya Kenya, Tanzania watacheza na timu ya Taifa ya Misri mapema
mwezi ujao ambapo mchezo wa awali utafanyika jijini Dar es salaam kati ya mwezi
Machi 7, 8 na marudiano kufanyika baada ya wiki moja nchini Misri.
Endapo timu ya
Taifa ya Tanzania itaiondoa timu ya Taifa ya Misri, moja kwa moja itakata
tiketi ya kushiriki Fainali za Mataifa Afrika kwa Soka la Ufukweni 2015
zinazotarajiwa kufanyika Visiwa vya Shelisheli kuanzia April 14 - 19 mwaka huu.
Kwa niaba ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), familia ya mpira na watanzania kwa
ujumla wanawapa pongezi timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la Ufukweni kwa
ushindi huo na kuwatakia maandalizi mema kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya
Misri.
0 comments:
Post a Comment