Tuesday, April 16, 2013
HUKUMU DHIDI YA WAFANYABIASHARA YA WATUMWA YAPUNGUA BARANI ULAYA
Ripoti ya kwanza ya Umoja wa Ulaya juu ya biashara ya kuwauza binaadamu inaonyesha kuwa kuhukumiwa kwa vinara wa biashara hiyo kumepungua wakati idadi ya watu wanaoingia katika mtego wa biashara hiyo haramu inaongezeka.
Kamishna wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya, Cecilia Malmstrom, amefahamisha juu ya matokeo hayo yaliyotokana na utafiti wa miaka mitatu.
Ujerumani na nchi nyingi za Umoja wa Ulaya zimeshindwa kuzitekeleza sheria kali zilizopitishwa na Umoja wa Ulaya ili kukabiliana na biashara ya binaadamu.
Ni nchi sita tu za Umoja wa Ulaya zilizoitekeleza sheria mpya dhidi ya biashara ya binaadamu. Maalfu ya watu wanakongwa na kuingia katika mtego wa wafanyabiashara ya kuuza binadamu kila mwaka.
Wengi wao ni wanawake wanaotumikishwa kama makahaba, lakini pia wanafanyishwa kazi ngumu na za kihalifu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment