Miongoni mwa nyota waliowahi kuitikisa dunia katika anga
za kimichezo ni Luis Figo.
Kuelekea katika mchezo
wa fainali wa Ligi ya Mabingwa kati ya Juventus dhidi ya
Barcelona,mchezaji nyota wa dunia Luis Figo ameondolewa katika kikosi
kitakachojumuisha wachezaji waliowahi kuvichezea vilabu vya Barcelona na Juventus.
Luis Figo amewahi kuichezea Barcelona kwa miaka mitano
kabla ya kuhamia klabu ya Real Madrid.
Kitendo cha kuhamia klabu ya Real Madrid kiliwachukiza
sana viongozi na mashabiki wa Barcelona kwa kumuita msaliti.
Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limeunda vikosi
viwili vya Barcelona na Juventus dhidi ya kikosi cha dunia katika mchezo wa
hisani .
Kikosi cha kwanza cha UEFA kimemjumuisha Luis Figo lakini
akapingwa vikali na viongozi wa Barcelona kuwepo katika kikosi hicho.
Mjumuisho wa kikosi cha Barcelona na Juventus
kitakachocheza na mastaa wengine wa dunia hiki hapa:
JUVENTUS NA BARCELONA MAGWIJI: Edwin van der Sar, Ciro Ferrara, Ludovic Giuly, Alessandro
Del Piero, Giovanni van Bronckhorst, Edmílson, Fabio Cannavaro, David
Trezeguet, Mark van Bommel, Gianluca Zambrotta, Deco, Eric Abidal, Christian
Vieri.
KIKOSI CHA DUNIA: Jens
Lehmann, Cafu, Youri Djorkaeff, Robert Pires, Predrag Mijatović, Giovane Elber,
Clarence Seedorf, Rai, Christian Karembeu, Steve McManaman, Pierre van
Hooijdonk, Marco Materazzi.
0 comments:
Post a Comment