Timu
ya yanga jana imeongeza pengo la point dhidi ya mpinzani wake Azam fc baada ya
kupata ushindi wa mabao matatu kwa moja mbele ya Mbeya City.
Yanga
sasa imefikisha alama 31 nne juu ya azam waliopo nafasi ya pili baada ya jana
usiku kulazimishwa sare ya bila kufungana na timu ya Prison kutoka mbeya mchezo
uliofanyika katika uwanja wa azam Complex Dar
es salaam.
Katika
mchezo wa jana wa Yanga timu hiyo iliruhusu goli katika lango lake baada ya
kuchezo michezo saba bila kuruhusu goli.
Magoli
ya yanga ya jana yalifungwa na Simon Msuva
katika
dakika ya 18 alipounganisha kwa kichwa krosi ya Oscar Joshua, magoli mengine
yalifungwa na Mrisho Ngassa na Amisi Tambwe.
Simon Msuva akishangilia bao lake la kwanza mbele ya timu ya Mbeya City
Tunawaua
kocha wa yanga Hans Van Pluijm akiteta na vijana wake
Ngassa akifanya yake sokoine
Mwenyekiti wa CHADEMA Freman Mbowe akiwasili uwanja wa Sokoine na mwenyeji wake mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi SUGU.
Ngassa akifunga bao la tatu la yanga
0 comments:
Post a Comment