Msimu wa pili wa mashindano ya mpira wa miguu kwa timu za
mtaani yajukanayo kama SPORTS XTRA
NDONDO CUP unatarajiwa kuanza mei 20 mwaka huu kwa hatua ya awali.
Mashindano hayo yamelazimika kuanzia hatua ya mtoano kutokana
na kujitokeza kwa timu nyingi zilizoomba kushiriki baada ya mwaka jana michuano
hiyo kufanya vizuri.
Hatua ya awali inatarajiwa kufikia tamati mwezi ujao kwa
kupatikana timu 16 miongoni mwa timu 81, ambazo zitaungana na timu nyingine 16
zilizofanikiwa kuingia hatua ya mtoano mwaka jana.
Katibu wa kamati ya mashindano ya DRFA Daud Kanuti ambaye
kimsingi ndiye mratibu wa mashindano hayo amezitaka timu shiriki kuheshimu
kanuni za mashindano.
Kanuti pia amezungumzia changamoto ya waamuzi ambayo
imekua ikibebeshwa lawama katika ligi mbalimbali kutokana na ukiukwaji wa
sheria kumi na saba za soka.
''uzuri ni kwamba drfa tuna waamuzi wengi na wamekua wanafanya vizuri hivyo hatua hofu na waamuzi wetu na tunaamin watafanya vizuri"alisema
Mashindano haya yalianzishwa mwaka jana na Clouds Media Group
kupitia kipindi chake bora cha michezo cha Sports Xtra kwa lengo la kutoa
nafasi kwa vijana wengi mitaani kuonesha vipaji vyao.
Michezo ya ufunguzi hapo kesho ni kati ya Vijibweni city
dhidi ya Wakung’aza Fc uwanja wa Mizinga, na Santiago Chile dhidi ya Kisarawe
Rangers pale shule ya Benjamin Mkapa.
Michezo mingine ni kati ya Faru Jeuri dhidi ya Kisarawe
United pale airwing Ukonga, na Sindano Fc na No Star uwanja wa Kinesi Sinza
0 comments:
Post a Comment