Rashid Mandawa akiwa ameshika tuzo ya mchezaji bora wa mwezi november baada ya kuipokea uwanja wa taifa.
Timu ya soka
ya Mwadui Fc imezidi kujiimarisha baada yah ii leo kukamilisha usajili wa
mchezaji mwingine wa Kagera Sugar Rashid Mandawa.
Mandawa ambaye
msimu wa ligi uliomalizika mwezi huu amefunga magoli kumi na kushika nafasi ya
nne kwenye msimamo wa wafungaji, amesaini mkataba wa mwaka mmoja na timu hiyo
ya mkoani Shinyanga.
Kabla ya
kusaini mkabata huo kulikua na taarifa kuwa huenda angejiunga na Simba au
kwenda Tp Mazembe kwa ajili ya majaribio.
Mandawa anakua
mchezaji wa pili kusajiliwa na timu hiyo baada ya juma lililopita mchezaji
mwenzake wa Kagera Sugar Maleges Mwanga.
0 comments:
Post a Comment