Baada ya kufanikiwa kuipandisha ligi kuu timu ya Mwadui Fc, Kocha Jamhuri Kihweli amesaini mkataba mwingine wa miaka mitatu na timu hiyo.
Kabla ya
kusain mkataba huo mchana wa leo, juzi kulikua na taarifa kuwa kocha huyo
hataendelea na timu hiyo baada ya kutokubaliana baadhi ya mambo.
Hata hivyo
baada ya kikao cha uongozi wa Mwadui Fc na JULIO hapo jana timu hiyo imeamua
kumuongezea mkataba wa miaka mitatu.
Julio baada
ya kuipandisha Mwadui mwanzoni mwa mwaka huu alienda kwa muda kuifundisha timu
ya Coastal Union aliyoinusuru kushuka daraja pamoja na kuweka rekodi ya
kufungwa magoli mengi kwenye ligi kuu, magoli 8 dhidi ya Yanga.
Haijafahamika
kama kocha huyo ataendelea kuwa na msaidizi wake Amri Said au atakua na
wasaidizi wengine.
0 comments:
Post a Comment