Ikulu ya Marekani na Idara ya
Habari (Maelezo), wametangaza ratiba ya Rais Barrack Obama atakapozuru
Tanzania huku ikionyesha kuwa atakaa siku mbili tu, kuanzia Julai Mosi
na kuondoka kesho yake.
Tanzania itakuwa nchi ya mwisho ya Afrika
kutembelewa na Obama baada ya Senegal na Afrika Kusini. Mara
atakapowasili na ndege yake kubwa ya Air Force One, Rais Obama atazindua
barabara mpya katika upande wa Mashariki wa geti la kuingia Ikulu.
Rais Obama, ambaye atafuatana mkewe Michelle pia
siku hiyohiyo atazungumza kwa nyakati tofauti na wafanyabiashara kutoka
nchi za Afrika na Marekani kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Dar es
Salaam.
“Pia amepanga kuzungumza na maofisa wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania,” ilisema taarifa ya Maelezo.
Baada ya shughuli hiyo, Rais Obama atahudhuria
dhifa ya taifa atakayoandaliwa Ikulu na mwenyeji wake, Rais Jakaya
Kikwete.
Siku itakayofuata ataweka shada la maua kwenye sehemu ulipokuwa Ubalozi wa Marekani ikiwa ni kumbukumbu ya watu waliofariki katika shambulizi la bomu mwaka 1998.
Pia atatembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion na atatoa hotuba akizungumzia mikakati ya Marekani ya kulisaidia Bara la Afrika kuzalisha nishati ya umeme.

“Tanzania ni mshirika muhimu wa Marekani,” alisema
Ofisa wa Ikulu ya Marekani, Ben Rhodes wakati alipozungumza na
waandishi wa habari mwishoni mwa wiki katika Ikulu ya Marekani kuhusu
ratiba ya ziara ya Obama barani Afrika.
Pia mke wa Obama atakuwa na ratiba yake. Julai
Mosi, atapata staftahi na mwenyeji wake, Salma Kikwete katika ofisi za
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), Dar es Salaam.
Pia atatembelea sehemu ubalozi wa zamani wa
Marekani na baadaye atashuhudia onyesho la utamaduni la Kikundi cha Baba
wa Watoto, ambacho kinajumuisha watoto wa mitaani wenye umri kuanzia
miaka mitano hadi 18 kwenye Makumbusho ya Taifa.
Julai 2, atahudhuria mkutano na wake wa marais wa nchi za Afrika ambao pia utahudhuriwa na mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush, Laura.
Chanzo mwananchi.
Julai 2, atahudhuria mkutano na wake wa marais wa nchi za Afrika ambao pia utahudhuriwa na mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush, Laura.
Chanzo mwananchi.
0 comments:
Post a Comment