Mahakama ya mji wa Milan nchini Italia imemuhukumu kifungo cha miaka saba jela, Silvio
Berlusconi Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo.
Berlusconi
ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Italia kwa vipindi vitatu tofauti, alipatikana na hatia ya kujihusisha na vitendo vya ngono na mabinti walio na umri wa chini ya miaka 18.
Mahakama hiyo pia imemfungia
Berlusconi mwenye umri wa miaka 76 kujishughulisha na masuala ya siasa kwa maisha yake yote baada ya kukumbwa na kashfa hiyo.
Hii ni mara ya tatu kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Italia kuhukumiwa katika kipindi cha miezi tisa iliyopita.
Mwezi Oktoba 2012 alihukumiwa kifungo cha miaka minne jela baada ya kupatikana na hatia ya kukwepa kodi na mwezi Disemba mwaka huohuo alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kwa kosa la kutumia ushahidi wa kunasa mazungumzo ya simu kinyume cha sheria.
Mahakama ya Milan imetangaza kuwa,
Berlusconi anayo haki ya kukata rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa.
ikumbukwe kuwa berlucconi ni rais wa club ya ac milan ya italia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment