Wakati watanzania wakiisubiri katika
mpya itoe muongozo wa namna ya uundaji na upatikanaji wa wabunge, mkongwe
mwingine wa muziki wa kizazi kipya nchini Anselm Tryphone Ngaiza aka Chief
Rumanyika aka Soggy Doggy Hunter amemuwashia taa nyekundu mbunge wa jimbo la
Segerea, Dar es Salaam kwa madai yakutaka kuchukua nafasi yake kupitia tiketi
ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, mwaka 2015.
Kupitia ukurasa wake wa facebook na
tweeter mkongwe huyo amefunguka ifuatavyo "Shikamoo Mbunge wa Segerea, Makongoro
Mahanga, imetosha sasa nadhani ni zamu yangu kuwatumikia wana-segerea 2015 kupitia CHADEMA".
Nikipiga nae story asbh ya leo
mkongwe huyo ambaye kwa hivi sasa ni mtangazaji wa radio ebony fm ya mkoani iringa amesema pamoja na kutuma ujumbe huo bado hajatangaza nia rasmi,
ameongeza kwa kusema kuwa wikiendi ijayo inaweza kuwa na picha rasmi ya kile
alichoandika kwenye mitandao ya kijamii.
Hatua ya Soggy ni muendelezo wa
msururu wa wanamuziki kuingia kwenye siasa baada ya kufunguliwa njia na Joseph
Mbilinyi aka Sugu ambaye kwa sasa ni mbunge wa jimbo la Mbeya mjini, mapema
mwezi uliopita mkali mwingine Joseph Haule aka Prof Jay alichukua kadi ya uanachama
wa CHADEMA na sasa ni zamu ya Soggy.
hapa soggy akisakata kwaito na wafanyakazi wenzake wa ebony fm
Pia wapo wananmuziki waliojiingiza
kwenye siasa kama Kala Pina aliyegombea nafasi ya udiwani katika uchaguzi wa
mwaka 2010 kupitia CUF, huku mkongwe wa bongo fleva kutoka Morogoro Afande Sele
akitajwa kujiunga na moja ya chama cha siasa ambacho akijawekwa wazi na
kugombea mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment