TIMU YA TAIFA YA TAHITI YAAMBULIA MAGOLI 24 KWENYE MICHEZO 3 KATIKA KOMBE LA MABARA NCHINI BRAZIL
Katika hatua ya mwisho ya michuano ya
makundi kwenye mashindano ya kombe la
mabara la Confederations Cup nchini Brazil
mabingwa wa dunia Uhispania
waliwaonyesha mabingwa wa Afrika, Nigeria
kandanda ya pasi fupi na kuwachapa mabao
matatu kwa bila.
Katika mechi nyingine Uruguay haikuwa na
huruma na Timu ya Tahiti ya wachezaji wa
ridhaa karibu wote.
Kwa mara nyingine Tahiti iligeuzwa kapu la
magoli kwa kuchabangwa mabao manane
kwa bila.
Uhispania na Uruguay zimeingia katika nusu
fainali, ambapo Uhispania itapambana na
Italia na Uruguay itamenyana na Brazil.
0 comments:
Post a Comment