Main Menu

Monday, June 24, 2013

AFYA YA RAIS MSTAAFU NELSON MANDELA YAZOROTA TENA, DUA ZENU ZAHITAJIKA

Afya ya Rais mstaafu wa Afrika kusini, Nelson  Mandela imezorota na sasa yumo katika hali mbaya. 


Taarifa hiyo imetolewa na serikali ya Afrika Kusini. 


Ofisi ya Rais Jacob Zuma imesema katika tamko kwamba Rais huyo alimtembelea Mandela  hospitalini hapo jana na aliarifiwa na wafanyakazi  wa hospitali juu ya kudhoofika kwa hali ya mpinga ubaguzi huyo maarufu, katika muda wa saa 24  zilizopita.


Mandela mwenye umri wa miaka 94 alipelekwa hospitali kiasi cha wiki mbili zilizopita kutokana na kurudiwa tena na maambukizi ya pafuni.


Rais Zuma amesema madaktari wanafanya kila linalowezekana ili kuirejesha afya yake na kwamba anaangaliwa vizuri sana.

0 comments:

Post a Comment