Kampuni ya Fenway Sports Group ya nchini Marekani ambao
ni wamiliki wa klabu ya Liverpool , imesema haina mpango wa kumfukuza kocha wa
klabu hiyo BRENDAN RODGERS kwa sasa.
Kocha huyo atakutana na Wamiliki wa Klabu hiyo mwishoni
mwa msimu , ili kutathmini maendeleo kwa kuangalia malengo ya Klabu na kama
malengo hayo yamefikiwa.
Msimu huu haujawa mzuri kwa Klabu ya Liverpool kutokana
na kushindwa kufuzu kucheza ligi ya mabingwa Barani Ulaya , lakini pia
kuondolewa katika hatua za nusu fainali ya michuano ya FA na kombe la Ligi.
Msimu uliopita Liverpool ilitumia zaidi ya euro milioni
100 kwa ajili ya usajili wa wachezaji wengi akiwemo MARIO BALOTTELI ,ADAM LALLANA, RICKIE LAMBERT, DEJAN LOVREN, DIVOCK ORIGI na
ALBERO MORENO toka Sevilla.
Wakati huohuo mshambuliaji wa Klabu hiyo RAHEEM STERLING
alijikuta akizomewa na mashabiki katika hafla ya utoaji wa tuzo za Klabu hiyo
hapo jana.
Mchezaji huyo alizomewa wakati akienda kuchukua tuzo yake
ya mchezaji bora mwenye umri mdogo wa Klabu hiyo.
Kuzomewa kwa mchezaji huyo kumekuja kipindi ambacho ,
anataka kuongezewa mkataba mpya , lakini pia huku akitishia kuondoka katika
klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment