Fainali ya kwanza ya ligi ya kikapu nchini Marekani- NBA
kwa Kanda ya Magharibi imeendelea tena leo
alfajiri kwa mchezo mmoja, kwa kuikutanisha timu ya Houston Rockets na
Golden State Warriors.
Katika mchezo huo,timu ya Golden State Warriors imepata
ushindi wa pointi 110 kwa pointi 106 za Houston Rockets.
Katika mchezo huo,STEPHEN CURRY wa Golden State Warriors
alifunga pointi 34 huku JAMES HARDEN akifunga pointi 28 kwa upande wa Houston
Rockets.
Kesho alfajiri kutachezwa mchezo mwingine wa fainali kwa
Kanda ya Mashariki kati ya Cleveland Cavaliers na Atlanta Hawks.
0 comments:
Post a Comment