Sports Xtra Ndondo Cup , mashindano ya mpira wa miguu kwa
timu za mitaani za jiji la dar es salaam
yameanza leo kwa hatua ya awali.
Michezo ya ufunguzi leo imefanyika katika viwanja vinne
vya Kinesi, Mizinga, Airwing na Benjamin Mkapa.
Katika michezo hiyo ya ufunguzi Vijibweni city wamekubali
kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Wakung’aza Fc katika dimba la mizinga
kigamboni.
Wazee wa vigoma Santiago Chile wametoa kipigo cha bao 3-0
kwa Kisarawe Rangers pale shule ya Benjamin Mkapa.
Faru Jeuri wakaishindilia Kisarawe United bao 4-0 pale jeshini
airwing Ukonga, na Sindano Fc ikachapwa 1-0 na No Star uwanja wa Kinesi Sinza.
Michezo hiyo itaendelea tena kesho kwa Mbagala city vs Mjivuni
fc, Tuamoyo fc vs Toangoma fc, Sharif united vs Kivule united na Faru Dume vs Kimara
united.
0 comments:
Post a Comment