Tuesday, May 19, 2015
RAHEEM STERLING KUIAGA LIVERPOOL IJUMAA
Mchezaji huyo anatarajiwa kukutana na Mkurugenzi wake Ian Ayre na kocha wake Rodgers siku ya ijumaa, kuwaeleza kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo.
Hata hivyo klabu ya Liverpool haijasema lolote kwa sasa ingawa inaonekana bado wanamhitaji mchezaji huyo kinda mwenye umri wa miaka 20 na ambaye mkataba wake unaisha mwaka 2017.
Klabu kadhaa zimeonyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo, ikiwemo klabu ya Manchester City, Arsenal na Real Madrid.
Hata hivyo Kaptain wa Liverpool Steven Gerrard amemtaka Sterling kubakia katika timu hiyo na kusisitiza kuwa “ni vizuri kuwa katika klabu ambayo kocha ana imani na wewe”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment