Kitendawili cha wapi kipa wa klabu ya Manchester United
David De Gea atacheza msimu ujao bado
hakijateguliwa, kutokana na uvumi unaoenea kuwa kipa huyo ataichezea klabu ya
Real Madrid msimu ujao.
Wakala wa David De Gea Jorge Mendez atafanya mazungumzo
na klabu ya Manchester United wiki hii kujua hatma ya mteja wake.
Wiki iliyopita kocha wa Manchester United Louis Van Gaal
alisema kuwa hatomzuia kipa huyo kujiunga na Real Madrid lakini endapo atapata
ofa nzuri toka kwa miamba hiyo ya Hispania.
Hali ya De Gea katika klabu ya Manchester United imekuwa
ya mashaka na mchezaji huyo amekuwa katika presha kubwa kutoka katika familia
yake inayoishi nchini Hispania.
Mchezaji huyo amekuwa na mfanikio makubwa sana katika
klabu ya Manchester United na kwakuutambua mchango wake, klabu ya Manchster
United imempa mkataba mwingine utakaomfanya kulipwa kiasi cha euro laki mbili
kwa juma.
Lakini De Gea bado anaonekana hayupo tayari kuendelea
kuishi nchini England.
Kwa upande wa Real Madrid,wapo tayari kumtoa kipa wake
Iker Cassilas ambaye uwezo wake umeonekana kupungua sana na kumchukua David De
Gea.
Kipa wa zamani wa klabu ya Manchester United Raimond Van
Der Gouw anaamini mrithi sahihi wa David De Gea katika klabu hiyo ni Victor
Valdes.
0 comments:
Post a Comment