Sports xtra day bonanza kwa jiji la
mwanza lilifanyika mwaishoni mwa juma lililopita na kuwashuhudia waandaaji clouds
media group wakitwaa ndoo ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake miaka
mitatu iliyopita.
Katika bonanza hilo lililofanyika
katika uwanja wa ccm kirumba lilishirikisha makampuni kumi ya jijini mwanza na
kuishuhudia The Dream Team ikiifumua Bank ya Nmb kwa mikwaju ya penalt 3-2
katika mchezo wa fainal.
Clouds iliiwatoa mabingwa wa mwaka
jana Dar es salaam Fastjet kwenye hatua
ya nusu fainal wakati NMB wao waliwatupa nje timu ya Cocacola.
Kampuni zilizoshiriki kwenye bonanza
hilo jijini mwanza ni SAUT, MEGA TRADE INVESTIMENT, NYANZA BOTLING CO LTD,
SONGORO MARINE, TCC, THAQAFA teachers, NMB, TBL MWANZA na mabingwa CLOUDS MEDIA
, GROUP.
Baada ya kumalizana na wakazi wa
mwanza sasa ni zamu ya jiji la mbeya wikiendi ijayo ya tarehe 23…jipangeeeee
0 comments:
Post a Comment