Dunia tunayoishi ina mambo mengi sana, yapo mambo ya
kufurahisha na mengine ya kusikitisha na kuhuzunisha.
Ipo mikasa mingi ya
kimaisha ambayo huwakumba wanamichezo na hata wale ambao wanandoto ya kuwa
wanamichezo wakubwa hapo baadae.
Embu fuatilia stori ya kijana Martunis
aliyenusurika na tetemeko la ardhi na sasa anategemea kuwa na ndoto za kuwa
mchezaji mkubwa duniani hapo baadae.
Martunis ni
kijana ambaye amezaliwa na kukulia katika eneo linalojulikana kama Banda Aceh nchi ya Indonessia.Mwaka 2004 kulitokea tetemeko kubwa sana lijulikanalo kama Tsunami katika ukanda wa bahari ya Indi na kuua watu takribani laki 230,000 katika nchi za ukanda wa bahari ya Indi ikiwepo Singapore.
Temeko hilo lilibadili sura na maisha ya Muritius kutokana na kumpoteza mama yake na kaka zake wawili.
Katika tetemeko hilo,Martunis naye alizolewa na maji na kusukumwa hadi beach na kujikuta amekaa kwenye dimbwi la maji karibu na bahari.
Alikaa hapo kwa muda wa siku 21 akila vyakula vilivyosombwa na maji kuletwa hapo alipo baada ya Tsunami kutokea.
Mauritius alikutwa hapo na kikundi cha waandishi wa Habari akiwa anashangaa ufukwe wa mji wa Indonesia akiwa amevaa jezi namba 10 ya mchezaji wa Ureno Rui Costa ambayo alikua amevaa wakati anasombwa na maji.
Alipelekwa hospitali na kutundikiwa dripu kwa sababu uchunguzi wa kitabibu ulionesha kuwa Martunis alikumbwa na ugonjwa wa ….Mmoja kati ya wanachama wa kikundi cha kuokoa watoto alisema kuwa endapo wangechelwa kumokoa kwa siku moja,basi Martunis angekutwa amekufa.
Alivyoulizwa kuhusu jinsi alivyonusurika kifo Martunis alisema kwamba “Nilikua siogopi kwa wakati ule kwasababu bado nilikua nataka kuendelea kuishi na kuwaona ndugu zangu na pia kuwa mcheza mpira”
Story yake iligusa nyoyo za watu wengi akiwemo mchezaji
wa Portugal Cristiano Ronaldo, Ronaldo
baada ya kujionea hali ya Muritius, alijitolea kwa kumlipia ujenzi wa nyumba yao mpya ambayo iliharibiwa na Tsunami.
Martunis
ameshakutana na Cristiano Ronaldo mara nyingi na hivi karibuni alikutana nae
mwaka 2013.
Mwaka 2005 Martunis alikutana na kikosi cha Ureno akiwemo shujaa
wake CR7 na akasema siku moja angependa kuchezea timu ya taifa ya Ureno.
Habari nzuri kwa sasa ni kwamba Martunis atacheza timu ya
under 19 akiwa na club ya Sporting Lisbon ambapo Cristiano Ronaldo alipitia.
Lisbon imesajili mchezaji huyo ambae toka kitambo alikua na ndoto za kucheza
soka ili awe kama nyota wa Ureno ambao ni Cristiano Ronaldo na Luis Figo.
Kituo cha vijana cha soka cha Sporting Lisborn kimewatoa
nyota wengi sana katika mchezo wa soka, Miongoni mwa nyota hao ni pamoja na
Cristiano Ronaldo, Luis Figo, Luis Nani, Erik Dier, Ricardo Quaresma, Simao, Joao
Moutinho, Jose Fonte, Nuno Valente, Silvestre Valera, Miguel Velso na Luis Boa
Morte.
Akizngumzia juu ya usajili wa chipukizi Muritius,Rais wa klabu
ya Sporting Lisbon Bruno De Carvalho
anasema” Martunis atafanya kazi katika kituo cha vijana cha Sporting
Lisbon.
Tutafanya kazi naye na kumuendeleza ili jae kuwa mtu mzuri katika na
mchezaji mkubwa katika klabu ya Sporting.
Kwa upande wake Martunis anasema kuwa” kucheza klabu ya
Sporting Lisbon ni ndoto ambayo imetimia.”
Kila la kheri Martunis katika maisha yako mapya kunako
klabu ya Sporting Lisbon.
0 comments:
Post a Comment