Taifa Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum
Lager kesho jumamosi saa 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki itashuka dimba
la Nakivubo kucheza na wenyeji Uganda.(The Cranes).
Mecho hiyo ya kesho ni mchez wa marudiano kuwania kufuzu
kwa fainali za CHAN mwaka 2016 zitakazofanyika mapema mwezi Januari nchini
Rwanda, mgeni rasmi atakua Rais wa Uganda Yoweri Mseveni.
Kikosi cha Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles
Mkwasa, kiliwasili jijini Kampala jana usiku na kimefikia katika hoteli ya
Grand Global iliyopo jirani na chuo kikuu cha Uganda Makerere.
Taifa Stars imefanya mazoezi leo jioni katika uwanja wa
Nakivubo yakiwa ni mazoezi mepesi na mwisho kuzoea uwanja kabla ya mchezo
wenyewe utakaofnayika kesho jioni.
Kocha Mkwasa akiongelea kuelekea mchezo huo amesema,
anashukuru vijana wake wamefika salama wote, hali nzao ni nzuri, morali ni ya
hali ya juu, kikubwa wanatambua wana deni kubwa kwa watanzania hivyo kesho
watapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
Akiongelea hali ya hewa na mazingira ya timu ilipofikia,
Mkwasa amesema hali ya hewa ni ya kawaida baridi na mvua kidogo haina tofauti
sana na Tanzania, mazingira ya hoteli ni mazuri na kusema kikubwa kilichobaki
ni kusaka ushindi katika mchezo huo na vijana wake wapo tayari.
Wakati huo huo mashabiki zaidi ya 50 kutoka nchini
Tanzania wanatarajiwa kuwasili kesho jumamosi alfajiri wakitokea jijini Dar es
salaam kuungana na watanzania wengine waishio nchini Uganda kuishangilia timu
ya Tanzania itakapokuwa ikipimbana na Uganda katika uwanja wa Nakivubo.
0 comments:
Post a Comment