Mwenyekiti
wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard kulia
akitoa msimamo wa wanahabari dhidi ya gazeti la Rai na mbunge
Msigwa leo ,kushoto ni katibu mtendaji wa IPC Francis Godwin
Wanahabari
Clement Sanga kushoto akiwa na mwakilishi wa New habari {2006} Ltd
wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania , Rai na Bingwa mkoa wa Iringa
Mercy Mwalusamba wakati wa kikao cha cha wanahabari mkoa wa Iringa
leo kujadili habari zilizoandikwa na gazeti la rai jumapili
WANAHABARI
mkoani Iringa wamekanusha vikali habari zilizoandika na gazeti la
Rai toleo namba 1067 la jumapili wiki iliyopita kuwa wanahabari mjini
Iringa wamehongwa fedha na viongozi wa CCM mkoa wa Iringa ili
wasiandike habari ya msaidizi wa mbunge Wiliam Lukuvi Bw Thom Malenga
kukamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na ujangili.
Wahanabari
hao katika kikao chao kilichofanyika leo katika ofisi za klabu
ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) mbali ya kukanusha
habari hizo kuwa zimeandikwa kwa lengo la kuchafua tasnia ya habari
mkoa wa Iringa ila bado wanalitaka gazeti la Rai na mbunge wa
jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa kuwataja waandishi
waliohongwa na viongozi wa CCM mkoa wa Iringa kabla ya wanahabari
hao hawajachukua hatua zaidi dhidi ya gazeti la rai pamoja na mbunge
Msigwa.
"Kilichoandikwa
na gazeti la Rai jumapili kuhusu wanahabari Iringa hawajatutendea
haki na wametuvunjia heshima yetu kwa wadau wa habari mkoa wa
Iringa na nje ya mkoa wa Iringa.....ila tunachotaka Rai kuwataja
waandishi hao waliohongwa ili sisi kwa sisi kama wanahabari
kuanza kuchukuliana hatua ....wakishindwa kufanya hivyo ndani ya
siku 14 kuanzia leo jumanne tutawafikisha baraza la habari Tanzania
(MCT)"
Walisema
wanahabari hao katika tamko lao la pamoja lililotolewa na
mwenyekiti wa IPC Frank Leonard kuwa taarifa hiyo imechafua vibaya
wanahabari Iringa na sio wacache ni wote kutokana na jinsi ambavyo
gazeti hilo lilivyoandika habari hiyo tena mbaya zaidi mwandishi wa
habari hiyo hakuweza kuwatendea haki wanahabari Iringa hata kwa
kuonyesha kuwahoji katika habari yake hiyo.
Leonard
alisema kuwa si kweli kama wanahabari Iringa walishindwa kuandika
habari hiyo ya kukamatwa kwa Malenga isipo kuwa wanahabari Iringa ni
makini na hawakutaka kuandika habari kwa kukurupuka hivyo walitaka
kabla ya kuandika kuweza kumpata msemaji wa kikosi hicho cha kupambana
na ujangili ili kulizungumzia hilo kabla ya kuandika jambo ambalo
wao kama wanahabari walikuwa wakilisikia mitaani bila kuwa na
uhakika.
Uandishi
wa habari mzuri ni pamoja na kuzingatia maadili ya uandishi na sio
kuandika bila ya kuwa na uhakika wa kile unachokiandika .
Hata
hivyo alisema kwa kuwa mbunge Msigwa amenukuliwa katika gazeti hilo
kama ndio msemaji wa jambo hilo wao kama wanahabari watamwandikia
barua mbunge huyo ili kusaidia kuwataja wanahabari waliohongwa pesa
vinginevyo wao kama wanahabari wa mkoa wa Iringa hawatamvumilia
mbunge Msigwa katika hilo .
Pia
alisema kuwa suala hilo kwa sasa ameachiwa mwanasheria wa IPC ili
kulifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwaandikia barua Rai na mbunge
Msigwa kuwataka kuthibitisha ukweli wa kilichoandikwa dhidi ya
wanahabari mkoa wa Iringa.
Na Francis Godwin Blog
0 comments:
Post a Comment