Mhe. Anne Makinda ( Mb),Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, akichangia uzoefu wa Tanzania katika ujenzi wa utawala wa kidemokrasia na ushirikishwaji wananchi na nafasi ya Bunge na wabunge katika ujenzi wa demokrasia hiyo ni katika mkutano uliokuwa ukijadili mada kuhusu utawala wa kidemokrasia na nafasi yake katika malengo ya maendeleo endelevu, Mhe. Spika alikuwa ni miongoni wa jopo hilo lilowashirikisha kutoka kushoto Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan. Eliasson, Balozi Pauel Seger wa Usiswi katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Anne Makinda, Balozi Eduardo Ulibarri wa Costa Rika katika Umoja wa Mataifa, Senator Aitzaz Ahsan kutoka Pakistan, na Ms. Gunilla Carlsson aliyewahi kuwa mjumbe mashuhuri kuhusu masuala ya ajenda za maendeleo baada ya 2015 na pia aliwahiki kuwa Waziri wa zamani wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Sweden
Mhe. Spika akisisitiza jambo katika siku ya pili ya mkutano wa mwaka wa maspika na wabunge kutoka mabunge mbalimbali duniani wakati walipokutana hapa Umoja wa Mataifa
Sehemu ya wabunge wakifuatiliana na kushiriki majadiliano hayom, aliyekaa kwenye kiti kirefu ni muongoza majadiliano, Nermeen Shaikh Mtangazani na mtayarishaji wa vipindi kuhusu masuala ya Demokrasia sasa
Mhe. Spika akibadilishana mawazo baadhi ya maafisa na wafanyakazi wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, wapo pia maafisa kutoka Wizara za fedha na Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa wanaohudhuria mijadala ya Kamati mbalimbali za Umoja wa Mataifa
Kusikiliza alichosema Mhe. Spika katika mkutano huu BOFYA MSHALE HAPO CHINI
0 comments:
Post a Comment