Rais kikwete baada ya kukabidhiwa mwenge wa uhuru
Rais akizungumza na viongozi wadini
Rais jakaya kikwete akiteta neno na mbunge wa Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa na mbunge viti maalum Chadema Chiku Abwao .
Vijana wa alaiki baada ya kumaliza onesho lao
Kilele cha mbio za mwenge wa uhuru
kimefikia tamati hii leo mkoani Iringa, Huku serikali ikiwa imeahidi kusimamia
miradi yote iliyozinduliwa ama kuwekwa jiwe la msingi.
Akihitimisha mbio hizo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amewashukuru Watanzania na vyombo vya habari kwa ushiriki wao katika kipindi chote cha kukimbizwa kwa mwenge wa uhuru.
Akihitimisha mbio hizo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete amewashukuru Watanzania na vyombo vya habari kwa ushiriki wao katika kipindi chote cha kukimbizwa kwa mwenge wa uhuru.
Akielezea janga la
ukimwi rais Kikwete amesema kuwa bado tatizo hilo
limeendelea kuwa kubwa katika mkoa wa Njombe ambao
unaongoza kwa maambukizi ukifuatiwa na mkoa wa Iringa kwa ambapo
amewataka wananchi wa mikoa hiyo kuendelea kuchukua
hatua ya kupunguza kasi ya maambukizi ya VVU na
kuendelea kutumia dawa ya kupumbaza virusi AVR’S inayotolewa na serikali huku wale ambao
hawajaathirika kuendelea kujilinda wasiathirike .
Ameongeza kuwa mwaka ujao ni mwaka
utakaokuwa na matukio makubwa matatu ya kusherehekea miaka 50
ya mapinduzi ya Zanzibar, miaka ya 50 ya muungano wa Tanganyika na
Zanzibar na kukamilika kwa katiba
mpya ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kama mambo yatakwenda
yalivyopangwa.
Aidha Rais Kikwete ameelezea nia ya serikali ya kuazimisha sherehe za kilele cha mwenge na siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julias Kambarage Nyerere kuwa ni kuyaenzi mawazo yake hususani kipindi hiki cha mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya.
Hata hivyo Rais Kikwete amesema kuna haja na umuhimu ukubwa wa kuanza kuadhimishwa siku ya kuzaliwa kwa hayata baba wa taifa kama njia sahihi ya kumuenzi na ipewe jina la nyerere day tofauti na ilivyo hivi sasa.
Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu zilizinduliwa rasmi na Rais wa Zanzibar, Dokta Ali Mohammed Shein, tarehe 6 May 2013 katika kijiji cha Chokocho Mkoa wa Kusini Pemba, ukiwa na kauli mbiu inayosema“Watanzania ni wamoja tusigawanywe kwa misingi ya tofauti za dini zetu, itikadi na rasilimali”.
picha kwa hisani ya mzee wa matukioblog
0 comments:
Post a Comment