Main Menu

Sunday, February 17, 2013

WAANDISHI WA HABARI MKOANI IRINGA WANOLEWA NAMNA YA KUZIMA MOTO


                   Kamanda wa jeshi la zimamoto mkoa wa iringa inspector kenned komba akitoa mafunzo kwa wanahabari mkoani humo.
                              aliyevaa t shirt nyeupe yahaya mohamedy wa ebony fm, ziada mnyawami na mpoki mwakapiso wafanyakazi wa manispaa ya iringa.

                             inspector komba na mwandishi wa iringa televishen vicent





                                 mwandishi wa habari wa gazeti la nipashe mkoani iringa mushi godfrey akizima moto katika mafunzo hayo.

Wananchi mkoani iringa wametakiwa kuachana na fikra kuwa jeshi la zimamoto na uokoaji lipo kwa ajili ya kushughulikia majanga ya moto pekee, na badala yake wametakiwa kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kuweza kuzuia majanga ya aina mbalimbali yanayoweza kujitokeza.

Kauli hiyo imetolewa na kamanda wa jeshi hilo mkoa wa Iringa Inspekta Kenned Komba wakati akitoa mafunzo kwa wanahabari ya namna ya kutumia vifaa vya kuzima moto pamoja na ushiriki wa vyombo hivyo katika kuwaelimisha wananchi.


Aidha Komba Amesema jeshi hilo limekua likihusika katika utoaji ushauri kwa wajenzi wa majengo marefu, pamoja na matumizi ya ya simu ya dharura inayotumiwa na jeshi hilo.


Hata hivyo pamoja na kudai kuwa jeshi hilo halina tatizo la vifaa na upungufu wa wafanyakazi, Komba amesema changamoto kubwa zinazowakabili ni kutoka kwa madereva pindi wanapoelekea kwenye tukio.

0 comments:

Post a Comment