Main Menu

Monday, October 14, 2013

CLUB YA MANCHESTER CITY YATANGAZA KUONGEZA UKUBWA WA UWANJA WAKE.


Klabu ya Manchester City inayoshiriki ligi kuu ya nchini England kupitia mkurugenzi wake imetangaza kuongeza ukubwa wa uwanja wao na kuufanya kuwa miongoni mwa viwanja vitatu vikubwa nchini humo.

Taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zimesema kuwa  upanuzi huo wa uwanja utatoka kuchukua watazamaji arobaini na nane elfu hadi kufikia sitini na moja elfu  na mwezi ujao mmiliki wa timu hiyo anataraji kupata majibu ya kibali cha kuongeza uwanja huo
.

Imeelezwa kuwa mara baada ya majibu kutolewa na uongozi wa jiji la Manchester mipango ya kuanza kwa ujenzi wa uwanja huo wa Itihadi itaanza kufanyika  mwezi wa pili mwakani.

Aidhaa taarifa hiyo imewatoa hofu mashabiki wa Machester City waliokata tiketi hadi  kipindi cha  zoezi hilo na upanuzi wa uwanja kwani  lengo ni kuongeza kipato cha timu hiyo inayofundishwa na kocha Manueli Pellegrin
.

0 comments:

Post a Comment