Tuzo ya Mo
Ibrahim ambayo hutolewa kwa Rais mstaafu aliyeonyesha uongozi mzuri barani Afrika, imeshindwa kutolewa kwa mara nyingine baada ya kukosa kiongozi aliyefanikiwa kuwa na vigezo vinavyotakiwa.
Hii ni mara ya pili tuzo hiyo kukosa mshindi ikiwa ni mara ya nne mfululizo tangu kuanzishwa kwake kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na viongozi wengi kushindwa kukamilisha masharti ya tuzo hiyo.
Katika mkutano na waandishi wa habari mjini London, uongozi wa tuzo hiyo umesema kuwa baada ya ukaguzi kufanyika hakuna hata kiongozi mmoja aliyestahili kutuzwa.
Tuzo hiyo ambayo hutolewa na mfanyabiashara bilionea mzaliwa wa Sudan na raia wa Uingereza, Mo
Ibrahim hutoa dola milioni 5 kwa kipindi cha miaka kumi na dola laki mbili kila mwaka hadi kiongozi huyo atakapofariki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment