Main Menu

Tuesday, October 29, 2013

KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, CHAFUNGULIWA JIJINI MBEYA LEO.


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto) akimpokea Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi cha siku tatu kinachofanyika katika Hoteli ya Paradise jijini Mbeya.

 Katika Hotuba yake ya ufunguzi, Ntunguja aliwaomba watendaji wakuu wa wizara hiyo washirikiane vizuri na watumishi wao ili kuleta mafanikio zaidi ndani ya wizara hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akizungumza na wajumbe wa baraza hilo kabla ya kufungua kikao cha siku tatu kinaofanyika 
 jijini Mbeya. Wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi.

 Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Edson Nyinyimbe. Wa pili kushoto ni Venance Ntiyalundura, Katibu wa tawi hilo. 

 Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi, 
Picha na Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani


0 comments:

Post a Comment