Ofa ya Klabu ya Liverpool ya
paun milioni 10 kwaajili ya kutaka kumsajili mlinzi wa kimataifa wa England Nathaniel Clyne imekataliwa na Southampton.
Clyne alijiunga na watakatifu hao akitokea Palace mwezi July mwaka 2012 mkataba wake unamalizika mwaka 2016.
Aidha Liverpool pia inatajwa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Burnley Danny Ings pamoja na kiungo wa Manchester City James Milner.
Msimu uliopita Liverpool iliigeuza Southampton gulio kwa kuwasajili Adam Lallana, Dejan Lovren na Rickie Lambert wote watatu kwa paun milion 50.
0 comments:
Post a Comment