Main Menu

Friday, March 29, 2013

RAIS KIKWETE AWAONGOZA MAOMBOLEZO YA ALIYEKUA MBUNGE WA CHAMBANI SALIM HEMED

Rais Jakaya Kikwete, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani CUF, Salim Hemed Khamis, aliyefariki dunia jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa baada ya kuuguaa ghafla wakati akiwa katika Kikao cha Kamati ya Bunge cha Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam juzi.

Katibu wa Bunge la Jamhuri, John Joel, akisalimiana na Samuel Sitta, katika Ukumbi wa Karimjee wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Salim Hemed Khamis.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya ndugu wa marehemu .
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakizungumza nje ya ukumbi wa Karimjee, baada ya kushiriki shughuli ya kuaga mwili wa marehemu.
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu,Salim Hemed Khamis, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Chambani Visiwani Pemba kupitia Chama cha CUF, aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakiingiza kwenye gari tayari kuelekea uwanja wa ndege kwa safari ya kuelekea Pemba kwa maziko, yatakayofanyika leo. 



Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete leo

ameongoza idadi ya wananchi na viongozi wa serikali waliojitokeza

kuuga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Chambani Pemba (CUF) Salum Hemed Khamis kilichotokea jana katika hospital ya taifa ya Mhimbili.



Wakiongea mara baada ya hitima fupi ya marehemu Spika wa bunge Anne Makinda na waziri wa ushirikiano wa Afrika mashariki Samwel Sitta ameelezea masikitiko yao na jinsi waliovyoondokewa na mbunge huyo ambae amefariki kwa ugonjwa wa shinikizo la damu.




Kwa upande wake naibu katibu Mkuu bara wa chama cha wananchi CUF Julias Mtatiro amesema kifo cha Salumu ni pengo kubwa kwa chama chao na amewataka wananchi wa jimbo lake kuwa watulivu mpaka hapo jitihada za kumtafuta atakaelithi nafasi yake zitakapoandaliwa.



Marehemu Salumu alizaliwa tarehe Septemba 20, 1951 shehia ya mizingani jimbo la chambani Pemba na hadi anaonja umauti, ameacha vizuka wawili na watoto wanane.

Picha na michuzi

0 comments:

Post a Comment