Wafanyakazi
wa Shirika la Habari la BBC wamegoma kupinga mpango wa kufutwa kazi wafanyakazi
katika shirika hilo.
Habari
zinasema kuwa, waandishi wa habari na wafanyakazi kadhaa wa BBC jana walifanya
mgomo wa masaa 12 kupinga mpango huo na kulalamikia mazingira magumu ya kazi
zao.
Washiriki wa
mgomo huo wametajwa kuwa, ni kutoka muungano wa Bectu na Muungano wa Taifa wa
Waandishi wa Habari wa Magazeti ambao wamepinga vikali mpango wa kupunguzwa
wafanyakazi katika shirika hilo.
Inatazamiwa
kwamba, mgomo humo utaathiri kwa kiasi kikubwa matangazo ya moja kwa moja ya
redio na televisheni ya Shirika hilo la Habari la BBC.
Zaidi ya
wafanyakazi 2000 watalazimika kufutwa kazi katika kipindi cha miaka mitano
ijayo, ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa kuwafuta kazi kwa lazima wafanyakazi
wa shirika hilo.
0 comments:
Post a Comment